JESHI la polisi nchini limeendelea kuandamwa na mzimu wa mauaji ya raia wasiokuwa na hatiai baada askari polisi aliyefahamika kwa jina moja la (Manase) kutuhumiwa kumpiga mwananchi na kusababisha kifo.
Tukio la polisi kumuua kijana huyo lilisababisha tafrani kubwa baina ya polisi na wananchi wenye hasira kali kwa kuvamia kituo hicho kwa lengo la kulipiza kisasi kwa kuchoma moto kituo hicho na kutaka askari aliyehusika na mauaji ya kijana huyo naye auwawe.
| Mbunge wa Bukombe Profesa, Kulikoyela Kahigi(kulia), CHADEMA, akipokea maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Bukombe Dk. Archard Rwezahura, aliyevaa shati la kitenge jinsi alivyopokea maiti ya kijana huyo ambaye alipigwa risasi na Polisi na kufikishwa hospitali hapo akiwa amefariki. |
>>>>Hata hivyo askari walilazimika kutumia nguvu nyingi kwa kurusha mabomu ya machozi, risasi za moto na risasi baridi kwa ajili ya kuwatawanya wananchi hao ambao walikuwa wakirusha mawe kwa lengo la kuwajeruhi askari hao na kuharibu mali za kituo hicho.
Tukio hilo lilitokana na askari ambao walikwenda kumkamata mtu ambaye anadaiwa kuwa ni jambazi na aliyesadikiwa kuwa alikuwa amejificha katika nyumba ambayo ipo katika mtaa wa kilimahewa mjini Ushirombo.
Ambapo askari hao walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na kumweka ndani ya gari. Baadhi ya wananchi walionekana kulizingira gari hilo huku wakitaka mtuhumiwa huyo atolewe kwenye gari ili auwawe.
Katika kukabiliana na hali hiyo askari walilazimika kufyatua risasi juu kwa lengo la kuwatawanya wananchi na ndipo askari mmoja alipo mlenga kijana huyo risasi ya kiunoni na kijana huyo kupoteza maisha hapo hapo.
