Friday, October 26, 2012

WANAOTUHUMIWA KUMUUA BARLOW WATAJWA



Majina hayo yametajwa na Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema amesema kuwa simu iliyoporwa ya mwanamama ambaye alikuwa akisindikizwa nyumbani na marehemu ndiyo imesaidia kukamilisha upelelezi huo na wahusika kukamatwa.

Waliotajwa kuhusika na hayo mauaji ni Muganyizi Michael Peter (36) ambaye ametajwa kwamba ndiye aliyemuua Barlow, Chacha Waitare Mwita (50), Magige Mwita Marwa (48),  Buganzi Edward Kusuta pamoja na Bhoke Marwa Mwita (42) ambao wote wamekatwa wakiwa Dar es Saalam walipokimbilia baada ya mauaji.

No comments:

Post a Comment