Sunday, November 25, 2012

BIFU ZITO POLISI NA FAMILIA YA MAREHEMU , USHIROMBO


HALI imezidi kuwa tete katika jeshi la polisi kituo cha Ushirombo kutokana na familia kuapa kulipiza kisasi kwa jeshi la polisi mjini hapo kutokana na mauaji ya kinyama ambayo yaliyofanywa na askari polisi kwa kumfyatulia risasi na kumuua hapo hapo kijana ambaye alifahamika kwa jina la Rashidi Juma (23).
Mauaji hayo ambayo yalifanyika juzi katika maeneo ya Kilima hewa kwa askari wa jeshi la polisi katika kituo cha Ushirombo Mkoani Geita ambaye amefahamika kwa jina la PC Emma G4 tofauti na ilivyokuwa imesemekana kuwa muuaji ni Manase familia kwa sasa imedai kuwa jeshi la polisi linatakiwa kuwajibishwa.
Mauaji hayo ambayo yalitokana na sakata la jeshi la polisi kumshika Mabura Mayala (40)ambaye anatuhumiwa kwa ujambazi kutokana na kujificha kati ya nyumba ambazo zipo maeneo hayo.
Kwa mujibu wa maelezo ya askari polisi pamoja na wananchi zinaeleza kuwa baada ya wananchi kubaini kuwa kuna mtu ambaye walimjengea mashaka walipiga simu polisi kwa lengo la kuomba masaada wa polisi ili akamatwe.
Hata hivyo habari zinasema kuwa baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo wananchi walianza kupiga kelele na kulitaka jeshi la polisi lililohusika na kumkamata mtuhumiwa huyo kumwacha ili wananchi waweze kujichukulia hatua ya kumpiga na kumuua jambo ambalo lisingekuwa rahisi kufanya hivyo.
Kwa mujibu wa shuhuda ambao waliona tukio hilo ndopo askari tajwa alipoamua kumlenga risasi kijana huyo ambaye alimpiga risasi katika sehemu ya nyonga na kumuua hapo hapo.

JESHI LA POLISi LAWAMANI TENA , ASKARI WAKE AUA


JESHI la polisi nchini limeendelea kuandamwa na mzimu wa mauaji ya raia wasiokuwa na hatiai baada askari polisi aliyefahamika kwa jina moja la (Manase) kutuhumiwa kumpiga mwananchi na kusababisha kifo.
Hali hiyo imejitokeza jana katika kituo cha polisi cha Ushirimbo Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, ambapo askari polisi alimpiga risasi na kumuua kijana ambaye alifahamika kwa jina la Rashid Juma (23).
Tukio la polisi kumuua kijana huyo lilisababisha tafrani kubwa baina ya polisi na wananchi wenye hasira kali kwa kuvamia kituo hicho kwa lengo la kulipiza kisasi kwa kuchoma moto kituo hicho na kutaka askari aliyehusika na mauaji ya kijana huyo naye auwawe.
Mbunge wa Bukombe Profesa, Kulikoyela Kahigi(kulia), CHADEMA, akipokea maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Bukombe Dk. Archard Rwezahura, aliyevaa shati la kitenge jinsi alivyopokea maiti ya kijana huyo ambaye alipigwa risasi na Polisi na kufikishwa hospitali hapo akiwa amefariki. 
>>>>Hata hivyo askari walilazimika kutumia nguvu nyingi kwa kurusha mabomu ya machozi, risasi za moto na risasi baridi kwa ajili ya kuwatawanya wananchi hao ambao walikuwa wakirusha mawe kwa lengo la kuwajeruhi askari hao na  kuharibu mali za kituo hicho.
Tukio hilo lilitokana na askari ambao walikwenda kumkamata mtu ambaye anadaiwa kuwa ni jambazi na aliyesadikiwa kuwa alikuwa amejificha katika nyumba ambayo ipo katika mtaa wa kilimahewa mjini Ushirombo.
Ambapo askari hao walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na kumweka ndani ya gari. Baadhi ya wananchi walionekana kulizingira gari hilo huku wakitaka mtuhumiwa huyo atolewe kwenye gari ili auwawe.
Katika kukabiliana na hali hiyo askari walilazimika kufyatua risasi juu kwa lengo la kuwatawanya wananchi na ndipo askari mmoja alipo mlenga kijana huyo risasi ya kiunoni na kijana huyo kupoteza maisha hapo hapo.

Tuesday, November 20, 2012

WACHIMBAJI MKOANI GEITA KUIBURUZA SERIKALI MAHAKAMANI


KIKUNDI cha umoja wa wachimbaji  wadogo wadogo wa madini ya dhahabu (Shilabela Gold Mining Co-operative Society  Limited) katika eneo la Lulembela Wilayani Bukombe Mkoani Geita wametishia kuiburuza serikali mahakamani kama hawatapewa leseni ya uchimbaji madini.
Hatua hiyo inatokana na kile ambacho wanasema kuwa inawezekana Ofisi za serikali zinaendeshwa kiujanja ujanja na utapeli hususani katika Wizara ya Nishati na Madini kwa kuwapendelea wachimbaji wakubwa na kuwakandaniza wachimbaji wadogo.
Akizungumza na Tanzania Daima Katibu wa umoja huo Felisian Anthony, alisema kuwa serikali kupitia Wizara ya nishati na Madini wanatakiwa kuingilia kati utoaji wa lesemi kwa wachimbaji hao kwani wametimiza vigezo vyote amavyo walitakiwa kutimiza kwa mujibu wa maelekezo ya maofisa Madini.
Alisema kunaonekana kuwepo kwa dalili mbaya ya kutaka kuwazunguka waombaji hao jambo ambali mpaka sasa linawafanya waombaji hao kukata tama na kujikuta wakiendelea kuwa masikini wa kutupwa wakati maeneo yao yana madini.
“Sisi ni wazawa na maeneo yetu yana madini na ndiyo maana tuliamua kutumia maeneo yetu kuomba kuchimba kwa kufuata taratibu zote lakini hapa kuna mchezo ambao unataka kuchezwa ili tusipate leseni ya uchimbaji na hili haliwezi kuvumilika “ alisema katibu.

Alisema kikundi hicho chenye wanachama zaidi ya 97 waliomba kuchimba madini katika maeneo ambayo ni mashamba yao kwa kuzingatia sera ya madini ya kumtaka mzawa ambaye yupo katika eneo lake akigundua kuwa kuna madini anaweza kufuata taratibu na kuweza kuchimba.
Kwa mujibu wa maelezo ya Anthony alisema kutoka na sera hiyo wanachama hao kwa kushirikiana walibaini maeneo yao ambayo wanaishi yalikuwa na madini ya dhahabu hivyo kuamua kufanya taratibu za kuomba leseni kama wachimbaji wadogo ili waanze kuchimba madini hayo wakiwa na matumaini ya kujikwamua kiuchumi.
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo walianza mchakato wa kufuatilia eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuomba usajili wa eneo hilo mwaka juzi (2011) na kufanikiwa kupata cheti cha usajili.
Alisema kuwa mnamo Ocktoba tisa 2011 walikwenda katika ofisi ya madini ya Kahama kwa ajili ya kupata utaratibu wa umilikaji wa eneo la uchimbaji wa madini na upatikanaji wa leseni.
Akitoa maelezo Katibu wa kikundi hicho alisema kuwa kutokana na juhudi zote na taratibu zilizofanywa na kikunbdi hicho Ofisa Madini Kutoka Kahama,aliyemtaja kwa jina la Nkya, alikubaliana na wanachimbaji hao na kuwataka walipie ada ya upimaji ambayo ilikuwa ni shilingi laki mbili abayo ililipwa kwa viwanja 10 ambavyo ni sawa na heka 50.

Sunday, November 11, 2012

VITA YA MEMBE NA BASHE NI DHAHIRI. BASHE ASEMA MEMBE NI MNAFIKI


MPASUKO ndani ya chama cha Maapinduzi CCM umeendelea kushika kasi jambo ambalo linawafanuya makada wa chama hicho kujikuta wakigawanyika kutokana na makundi hayo ambayo kwa sasa yanashika kasi.
Hali hiyo imejidhiilisha jana baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Husein Bashe kumtuhumu waziwazi,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano waa Kimataifa, Bernardi Membe kuwa ni kati ya wanasiasa wachache ambao wanashiri kutumia makundi ndani ya chama ili kuwachafua wengine.

Bashe akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa alisema kuwa analazimika kumtaja Membe kuwa ni kiongozi mnafiki ndani ya chama kutokana na kutokuwa na msimamao na kujenga chuki kati ya wana CCM wenzake.

Alisema kuwa Membe amekuwa mtaabishaji ndani ya chama kwani amekuwa akifanya siasa za kihuni na za kutengeneza makundi kutokana na hali hiyo Baashe alimtaja Membe kma muhumi, mnafiki na kiongozi ambaye ana sifa ya kushika madaraka ndani ya chama hicho kikongwe.

Bashe alienda mbali zaidi na kudai kuwa Membe amekuwa akiwatumia vibaraka wake ambao kimsingi hawana akiri za kufikiria akiwemo Naaibu Waziri wa Malisili na Utali Lazaro Nyalandu ambaye wanashikiana kufanyua hujuma ndani ya chama cha Maapinduzi.

Hata hivyo alisema kuwa Membe amekuwa na fikra za kukihujumu chama hichjo na kuandaa mazingira ambayo yatasababisha chi kuchukuliwa na upinzani katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Aidha Bashe alisema kuwa inaonyesha wazi kuwa Membe ni mwanasiasa ambaye amezoea kubebwa katika chaguzi mbalimbali na hata amekuwa kiongozi nadani ya CCM akisababbisha kuwepo kwa migongano ikiwa ni pamoja na kufanya siasa za kinafi na uongo ambazo amekuwa akizifanya ndani ya chama na kusababisha migogoro mikubwa hususani katika Jumuiya ya Vijana.

JK ANG'AKA MAKUNDI NDANI YA CCM


BAADA ya Chama Cha Mapinduzi kuonekana kinatajwa kwa kira mara na kujingezea umaarufu wa kutoa rushwa katika chaguzi zake sasa Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye pia ni Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, amefunguka na kutangaza msimamo wa kuwashighulikia wanachama ambao wananunua uongozi kwa kutoa rushwa kwa wajumbe ambao ni wapiga kura.
 Kufunguka kwa Mwenyekiti wa chama hicho huyo kunatokana kuwa takribani wiki moja sasa, makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamekuwa wakipigana vita ya wazi dhidi ya kundi linalotajwa kumuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani,Edward Lowassa, linalotaka kufanya mapinduzi ya safu ya juu ya uongozi ndani ya chama hicho.
Makundi hayo yanatokana na mwendelezo wa vita ya makundi hasimu ndani ya chama hicho ambayo yalianza mikakati ya kuhakikisha yanashika nafasi zote nyeti kuanzia ngazi za chini hadi taifa.
Hali hiyo inatokana na kujipanga ama kupanga safi ambayo itaweza kufanikisha uchaguzi mkuu wa ndani wa CCM katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2015.
Duru za uchunguzi za Tanzania Daima wakati mchakato wa kumtafuta Mwenyekiti CCM Taifa zimebaini kuwa, rais Kikwete baada ya kufikishiwa taarifa za kuwepo mpango wa kumpoka nafasi ya uenyekiti kwa kisingizio cha kumpungumzia majukumu unaodaiwa kuratibiwa na kundi la wana CCM wanaomuunga mkono,  Lowassa huku lengo halisi la hatua hiyo likiwa ni mkakati wa kundi hilo kujiimarisha katika kutoa mgombea urais kwenye uchaguzi wa 2015, aliamua kuitumia hotuba yake ya jana ya kufungua mkutano mkuu wa nane wa chama kuonya kuhusu jambo hilo na kuwataka wanaoutamani urais kutokiua chama hicho.

Thursday, November 8, 2012

MAKINDA: WABUNGE HAWAJUI KUULIZA MASWALI YA KISERA


KATIKA hali isiyo kuwa ya kawaida Spika wa bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda amewakemea na kuwabea wabunge kuwa hawna hoja za kuuliza katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Wazri Mkuu kutokana na wabunge wengi kushindwa kuuliza maswali ya kisera.
Makinda alisema katika kipindi cha Maswali ya Waziri Mkuu wabunge wanatakiwa kuuliza maswali ambayo yatakuwa ni ya kisera badala ya kuuliza maswali yao ya kijimbo ambayo kimsingi yanakwenda kinyume na kanuni za kumuuliza Waziri Mkuu maswali.
Kauli ya makinda imetokana na badhi ya wabunge kushindwa kuuliza maswali ya msingi ambayo alitakiwa kuulizwa Waziri Mkuu katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo .
Spika alisema kuwa kimsingi maswali ya leo (Jana) maswali mengi ya wabunge yalikuwa hayaeleweki na hayakuwa mazuri kwa waziri mkuu na badala yake yalikuwa yakiulizwa kwa kuzunguka saba bila kwenda moja kwa moja katika swali la msingi.
“Janani wabunge leo maswali yote yalikuwa mabaya sana wala hayakuwa mazuri kwani wabunge mekuwa mizungumza kwa kuzunguka na wakati mwingine mlikuwa kushindwa kuuliza, wabunge mmeshindwa kupanga vizuri maswali yenu lakini sasa mjifunze kuuliza maswali vizuri ili muweze kuelewa maswali ya msingi” alisema.
Hata hivyo alimtaka mbunge wa Bukombe Profesa Kulikoyera Kahigi, (Chadema),kumwandikisa waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu kuwepo kwa migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na maofisa wa malisili kuwanyanyasa wananchi ambao wanakadiriwa kufika 70,000.

KAFULILA : CCM INAKIUKA ILANI YAKE


MBUNGE wa Kigoma Kusini David Kafulila (NCCR-Mageuzi),amemchachafa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa kusema kuwa serikali inayoongozwa na Chama cha mapinduzi imekuwa ikigawa ikikiuka ilani ya chama chao ambayo inaelekeza kwa ardhi ni ishara ya ujamaa na badala yake wamekuwa wakiwabeba mabepari kutoka nchini marekani ambao wanapatiwa ardhi huku wazawa wakinyanyaswa.
 Kafulila aliitoa kauli hiyo jana bungeni bungeni wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, kwa kuhoji ni kwanini serikali imekuwa ikitumia mfumo wa kibeneru katika ugawaji wa ardhi kwa wawekezaji na kusahau kuwa ardhi kwa Tanzania ni hishara ya ujaamaa.
Mbali nahilo alitaka kuelewa ni kwanini wawekezaji wamekuwa wakipewa ardhi kubwa wakati wenyeji wakifukuzwa katika maeneo yao kwa ajili ya kuwapatia ardhi hiyo wageni hususani pale inapobainika kuwa ardhi hiyo ina rutuba.
Mbunge huyo alitolea mfano katika jimbo la kigoma kusini ambapo mwekezaji ambaye alimtaja kwa jina la Agrosol kupewa hekta 10,000 wakati eneo hilo ambalo alipewa mwekezaji huyo ambapo eneo hilo linakusudiwa kujengwa makao makuu ya halmashauri.
Aidha alimtaja mwekezaji mwingine kuwa ni FELISA kupewa hekta 3000.jambo ambalo lilipelekea kikosi cha mgambo wa mwekezaji huyo kuwapiga wananchi na kuwapeleka katika kituo cha jeshi la polisi na kusababisha wakazi hao kufunguliwa kesi katika mahakama ya mwanzo ya Mwandiga.
Kwa mujibu wa maelezo ya Kafulila alisema kutokana na serikali kuwa na tabia ya kuwapa kipaumbele wawekezaji wakubwa kupewa ardhi huku wazawa wanaendelea kutaabika kunaweza kutokea machafuko makubwa ambayo yatakuwa yamesababishwa na serikali yenyewe.

PINDA: KATIBA MPYA NI KABLA YA UCHAGUZI WA 2015

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda jana ameliahakikishia bunge kuwa ifikapo uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 tayari katiba mpya itakuwa imekamilika.
Pinda alitoa kauli hiyo kutokana na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe (Chadema),kuitaka serikali kutoa kauli bungeni ni lini itafanya marekebisho ya katiba kuhusu kurekebisha daftari la kudumu la mpiga kura.
Mbowe alisema kuwa kutokana na daftari lakudumu la mpiga kura kupitwa na wakati kunapelekea watanzania wengi kukosa haki yao ya kupiga kura katika chaguzi mbalimbali ambazo zinaendelea tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliopita.
Hata hivyo alimtaka Wazri Mkuu kutoa kauli ya serikali kama kuna mpango wowote wa kufanya marekebisho ya baadhi ya sheria zinazoongoza uchaguzi iwapo katiba mpya ambayo inakusudiwa kutumika mwaka 2015 itakuwa bado haijakamilika.
Mbowe alisema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa katiba mpya ambayo inatakiwa kuandikwa na kutumika katika mwaka 2015 na iwapo marekebisho hayo hayatafanyiwa marekebisho ni ya sheria ya uchaguzi kuna watu wengi watakosa haki zao za kupiga kura kama ilinavyojionyesha katika chaguzi ndogo.