Friday, December 7, 2012

TAZAMA NA UTAFAKARI!!!!!

MAIGIZO YA MAISHA YETU KIBONGO BONGO


Hawa hapa ni wazee wa kikiji kimojawapo katika Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, walikuwa katika mkutano wa wazi wa kisiasa uliofanywa chini ya uongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema, lakini wazee awa kabla ya kuanza kwa mkutano walianza maigizo kwa lengo la kutoa elimu juu ya wananchi jinsi wanavyonyanyasika kutokana na baadhi ya viongozi serikalini kuwa mafisadi na hapo wanaonyesha jinsi maisha ambavyo ni mabaya kwa watu ambao wanaishi vijiji huku mafisadi wanapeta mwome mzee mmoja ana mvi na anaonyesha maisha yake yalivyo mazuri na mwingine maisha yake ndo hivyo tena mwisho wanasema viongozi mafisadi ni sawa na mashetani

Thursday, December 6, 2012

NYUMBA ZETU BAADA YA MADINI KUANZA KUCHIMBWA KIJIJINI KWETU

NUKUU...."KAKA KARIBU HIZI NI NYUMBA ZETU NZURI TUMEJENGEWA NA SERIKALI YA KIKWETE AMBAYO INASEMA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA TULIACHA NYUMBA ZETU MBAYA KUPISHA MWEKEZAJI WA MADINI MGODI WA GGM NA SERIKALI IMEBORESHA MAISHA YETU KWA KUTUJENGEA NYUMBA HIZI TUNAMSHUKURU KIKWETE HAPA NI MKOA WA GEITA WENYE MADINI MENGI, HAYO NI MANENO YA DADA HUYU AMBAYE ALIFUKUZWA PAMOJA NA WENZAKE ZAIDI YA KAYA 86 KWA AJILI YA KUPISHA MWEKEZAJI DADA HUYU ANASEMA TANGU MWAKA 2007 WANAISHI MAISHA YA JINSI HIYO HUKU WASIJUE HATIMA YA MAISHA YAO KAMA HAITOSHI WATOTO SASA HAWAENDI SHULE. JAMANI HII NI SERIKALI YA VIONGOZI SIKIVU , NAIPENDA TANZANIA NAUPENDA UPOLE WA WATANZANIA NATAMANI ELIMU INGEKUWA KUBWA TAFAKARI NDG"
UNAWEZA KUKUBALIANA NA MIMI KUWA ALIYESHIBA HAMJUI MWENYE NJAA, BIBI HUYU ALIKUWA NA ASHAMBA MIFUGO, NYUMBA NZURI NA MAISHA YAKE NA FAMIIA YAKE YALIKUWA MAZURI, MWAKA 2007 UONGOZI WA MKOA WA GEITA KWA KUSHILIKIANA NA MGODI WA DHAHABU WA GEITA(GGM) ULIWATAKA WANANCHI AMBAO WALIKUWA NA MALI ZAO KUONDOKA MARA MOJA KUPISHA MGODI HUO, KWA AHADI KUWA WATALIPWA LAKINI CHA KUSIKITISHA HADI LEO HAKUNA FIDIA YOYOTE NYUMBA ZAO NDO HAYO MAHEMA MWONE BIBI AMBAYE ALIKUWA NA MAISHA MAZURI SASA ANAISHI KAMA MKIMBIZI KATIKA NCHI YAKE, ZAIDI MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA GEITA BW,ALLI KIDWAKA ANASEMA HAJUI KAMA KUNA WATU WANAOISHI KATIKA MAHEMA MABOVU KAMA HAYA LAKINI ANAJUA KUWA WANADAI NA KUNA MIGOGORO MINGI JAMANI TANZANIA TANZANIA WATU WANAKUFA NA KUTESEKA KWA AJILI YA WAWEKEZAJI TAFAKARI
JAMANI WATOTO UKIONA HAPA UTADHANI NI MAIGIZO LAKINI NI NYUMBA YA KUISHI WATU NA WATOTO AWA WANAISHI KATIKA NYUMBA HIZO HATA HIVYO AWANA FURSA YA KWENDA SHULE SI KWAMBA WALIZALIWA HAPO BALI WALIPISHA UCHIMBAJI WA MADINI YA MGODI WA DHAHABU GEITA GGM TANGU 2007 HADI LEO HAKUNA LOLOTE WALILOFANYIWA JAMANI TAFAKARI KAMA ANGEKUWA MWANAO.

SANAA NA UBUNIFU, PANZI WA KUCHONGWA HUYU HAPA


Huyu ni panzi wa kuchonga anapatikana katika mji mdogo wa Ushirombo,Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita kwa sasa mnaweza kuagiza kwa ajili ya mapambo kwa mawasiliano zaidi nipigie simu ama tumia mtandao