Friday, December 7, 2012
MAIGIZO YA MAISHA YETU KIBONGO BONGO
Hawa hapa ni wazee wa kikiji kimojawapo katika Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, walikuwa katika mkutano wa wazi wa kisiasa uliofanywa chini ya uongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema, lakini wazee awa kabla ya kuanza kwa mkutano walianza maigizo kwa lengo la kutoa elimu juu ya wananchi jinsi wanavyonyanyasika kutokana na baadhi ya viongozi serikalini kuwa mafisadi na hapo wanaonyesha jinsi maisha ambavyo ni mabaya kwa watu ambao wanaishi vijiji huku mafisadi wanapeta mwome mzee mmoja ana mvi na anaonyesha maisha yake yalivyo mazuri na mwingine maisha yake ndo hivyo tena mwisho wanasema viongozi mafisadi ni sawa na mashetani
Thursday, December 6, 2012
NYUMBA ZETU BAADA YA MADINI KUANZA KUCHIMBWA KIJIJINI KWETU
NUKUU...."KAKA KARIBU HIZI NI NYUMBA ZETU NZURI TUMEJENGEWA NA SERIKALI YA KIKWETE AMBAYO INASEMA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA TULIACHA NYUMBA ZETU MBAYA KUPISHA MWEKEZAJI WA MADINI MGODI WA GGM NA SERIKALI IMEBORESHA MAISHA YETU KWA KUTUJENGEA NYUMBA HIZI TUNAMSHUKURU KIKWETE HAPA NI MKOA WA GEITA WENYE MADINI MENGI, HAYO NI MANENO YA DADA HUYU AMBAYE ALIFUKUZWA PAMOJA NA WENZAKE ZAIDI YA KAYA 86 KWA AJILI YA KUPISHA MWEKEZAJI DADA HUYU ANASEMA TANGU MWAKA 2007 WANAISHI MAISHA YA JINSI HIYO HUKU WASIJUE HATIMA YA MAISHA YAO KAMA HAITOSHI WATOTO SASA HAWAENDI SHULE. JAMANI HII NI SERIKALI YA VIONGOZI SIKIVU , NAIPENDA TANZANIA NAUPENDA UPOLE WA WATANZANIA NATAMANI ELIMU INGEKUWA KUBWA TAFAKARI NDG"
UNAWEZA KUKUBALIANA NA MIMI KUWA ALIYESHIBA HAMJUI MWENYE NJAA, BIBI HUYU ALIKUWA NA ASHAMBA MIFUGO, NYUMBA NZURI NA MAISHA YAKE NA FAMIIA YAKE YALIKUWA MAZURI, MWAKA 2007 UONGOZI WA MKOA WA GEITA KWA KUSHILIKIANA NA MGODI WA DHAHABU WA GEITA(GGM) ULIWATAKA WANANCHI AMBAO WALIKUWA NA MALI ZAO KUONDOKA MARA MOJA KUPISHA MGODI HUO, KWA AHADI KUWA WATALIPWA LAKINI CHA KUSIKITISHA HADI LEO HAKUNA FIDIA YOYOTE NYUMBA ZAO NDO HAYO MAHEMA MWONE BIBI AMBAYE ALIKUWA NA MAISHA MAZURI SASA ANAISHI KAMA MKIMBIZI KATIKA NCHI YAKE, ZAIDI MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA GEITA BW,ALLI KIDWAKA ANASEMA HAJUI KAMA KUNA WATU WANAOISHI KATIKA MAHEMA MABOVU KAMA HAYA LAKINI ANAJUA KUWA WANADAI NA KUNA MIGOGORO MINGI JAMANI TANZANIA TANZANIA WATU WANAKUFA NA KUTESEKA KWA AJILI YA WAWEKEZAJI TAFAKARI
JAMANI WATOTO UKIONA HAPA UTADHANI NI MAIGIZO LAKINI NI NYUMBA YA KUISHI WATU NA WATOTO AWA WANAISHI KATIKA NYUMBA HIZO HATA HIVYO AWANA FURSA YA KWENDA SHULE SI KWAMBA WALIZALIWA HAPO BALI WALIPISHA UCHIMBAJI WA MADINI YA MGODI WA DHAHABU GEITA GGM TANGU 2007 HADI LEO HAKUNA LOLOTE WALILOFANYIWA JAMANI TAFAKARI KAMA ANGEKUWA MWANAO.
SANAA NA UBUNIFU, PANZI WA KUCHONGWA HUYU HAPA
Huyu ni panzi wa kuchonga anapatikana katika mji mdogo wa Ushirombo,Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita kwa sasa mnaweza kuagiza kwa ajili ya mapambo kwa mawasiliano zaidi nipigie simu ama tumia mtandao
Sunday, November 25, 2012
BIFU ZITO POLISI NA FAMILIA YA MAREHEMU , USHIROMBO
HALI imezidi kuwa tete katika jeshi la polisi kituo cha Ushirombo kutokana na familia kuapa kulipiza kisasi kwa jeshi la polisi mjini hapo kutokana na mauaji ya kinyama ambayo yaliyofanywa na askari polisi kwa kumfyatulia risasi na kumuua hapo hapo kijana ambaye alifahamika kwa jina la Rashidi Juma (23).
Mauaji hayo ambayo yalifanyika juzi katika maeneo ya Kilima hewa kwa askari wa jeshi la polisi katika kituo cha Ushirombo Mkoani Geita ambaye amefahamika kwa jina la PC Emma G4 tofauti na ilivyokuwa imesemekana kuwa muuaji ni Manase familia kwa sasa imedai kuwa jeshi la polisi linatakiwa kuwajibishwa.
Mauaji hayo ambayo yalitokana na sakata la jeshi la polisi kumshika Mabura Mayala (40)ambaye anatuhumiwa kwa ujambazi kutokana na kujificha kati ya nyumba ambazo zipo maeneo hayo.
Kwa mujibu wa maelezo ya askari polisi pamoja na wananchi zinaeleza kuwa baada ya wananchi kubaini kuwa kuna mtu ambaye walimjengea mashaka walipiga simu polisi kwa lengo la kuomba masaada wa polisi ili akamatwe.
Hata hivyo habari zinasema kuwa baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo wananchi walianza kupiga kelele na kulitaka jeshi la polisi lililohusika na kumkamata mtuhumiwa huyo kumwacha ili wananchi waweze kujichukulia hatua ya kumpiga na kumuua jambo ambalo lisingekuwa rahisi kufanya hivyo.
Kwa mujibu wa shuhuda ambao waliona tukio hilo ndopo askari tajwa alipoamua kumlenga risasi kijana huyo ambaye alimpiga risasi katika sehemu ya nyonga na kumuua hapo hapo.
JESHI LA POLISi LAWAMANI TENA , ASKARI WAKE AUA
JESHI la polisi nchini limeendelea kuandamwa na mzimu wa mauaji ya raia wasiokuwa na hatiai baada askari polisi aliyefahamika kwa jina moja la (Manase) kutuhumiwa kumpiga mwananchi na kusababisha kifo.
Hali hiyo imejitokeza jana katika kituo cha polisi cha Ushirimbo Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, ambapo askari polisi alimpiga risasi na kumuua kijana ambaye alifahamika kwa jina la Rashid Juma (23).
Tukio la polisi kumuua kijana huyo lilisababisha tafrani kubwa baina ya polisi na wananchi wenye hasira kali kwa kuvamia kituo hicho kwa lengo la kulipiza kisasi kwa kuchoma moto kituo hicho na kutaka askari aliyehusika na mauaji ya kijana huyo naye auwawe.
Mbunge wa Bukombe Profesa, Kulikoyela Kahigi(kulia), CHADEMA, akipokea maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Bukombe Dk. Archard Rwezahura, aliyevaa shati la kitenge jinsi alivyopokea maiti ya kijana huyo ambaye alipigwa risasi na Polisi na kufikishwa hospitali hapo akiwa amefariki. |
>>>>Hata hivyo askari walilazimika kutumia nguvu nyingi kwa kurusha mabomu ya machozi, risasi za moto na risasi baridi kwa ajili ya kuwatawanya wananchi hao ambao walikuwa wakirusha mawe kwa lengo la kuwajeruhi askari hao na kuharibu mali za kituo hicho.
Tukio hilo lilitokana na askari ambao walikwenda kumkamata mtu ambaye anadaiwa kuwa ni jambazi na aliyesadikiwa kuwa alikuwa amejificha katika nyumba ambayo ipo katika mtaa wa kilimahewa mjini Ushirombo.
Ambapo askari hao walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na kumweka ndani ya gari. Baadhi ya wananchi walionekana kulizingira gari hilo huku wakitaka mtuhumiwa huyo atolewe kwenye gari ili auwawe.
Katika kukabiliana na hali hiyo askari walilazimika kufyatua risasi juu kwa lengo la kuwatawanya wananchi na ndipo askari mmoja alipo mlenga kijana huyo risasi ya kiunoni na kijana huyo kupoteza maisha hapo hapo.
Tuesday, November 20, 2012
WACHIMBAJI MKOANI GEITA KUIBURUZA SERIKALI MAHAKAMANI
KIKUNDI cha umoja wa wachimbaji wadogo wadogo wa madini ya dhahabu (Shilabela Gold Mining Co-operative Society Limited) katika eneo la Lulembela Wilayani Bukombe Mkoani Geita wametishia kuiburuza serikali mahakamani kama hawatapewa leseni ya uchimbaji madini.
Hatua hiyo inatokana na kile ambacho wanasema kuwa inawezekana Ofisi za serikali zinaendeshwa kiujanja ujanja na utapeli hususani katika Wizara ya Nishati na Madini kwa kuwapendelea wachimbaji wakubwa na kuwakandaniza wachimbaji wadogo.
Akizungumza na Tanzania Daima Katibu wa umoja huo Felisian Anthony, alisema kuwa serikali kupitia Wizara ya nishati na Madini wanatakiwa kuingilia kati utoaji wa lesemi kwa wachimbaji hao kwani wametimiza vigezo vyote amavyo walitakiwa kutimiza kwa mujibu wa maelekezo ya maofisa Madini.
Alisema kunaonekana kuwepo kwa dalili mbaya ya kutaka kuwazunguka waombaji hao jambo ambali mpaka sasa linawafanya waombaji hao kukata tama na kujikuta wakiendelea kuwa masikini wa kutupwa wakati maeneo yao yana madini.
“Sisi ni wazawa na maeneo yetu yana madini na ndiyo maana tuliamua kutumia maeneo yetu kuomba kuchimba kwa kufuata taratibu zote lakini hapa kuna mchezo ambao unataka kuchezwa ili tusipate leseni ya uchimbaji na hili haliwezi kuvumilika “ alisema katibu.
Alisema kikundi hicho chenye wanachama zaidi ya 97 waliomba kuchimba madini katika maeneo ambayo ni mashamba yao kwa kuzingatia sera ya madini ya kumtaka mzawa ambaye yupo katika eneo lake akigundua kuwa kuna madini anaweza kufuata taratibu na kuweza kuchimba.
Kwa mujibu wa maelezo ya Anthony alisema kutoka na sera hiyo wanachama hao kwa kushirikiana walibaini maeneo yao ambayo wanaishi yalikuwa na madini ya dhahabu hivyo kuamua kufanya taratibu za kuomba leseni kama wachimbaji wadogo ili waanze kuchimba madini hayo wakiwa na matumaini ya kujikwamua kiuchumi.
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo walianza mchakato wa kufuatilia eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuomba usajili wa eneo hilo mwaka juzi (2011) na kufanikiwa kupata cheti cha usajili.
Alisema kuwa mnamo Ocktoba tisa 2011 walikwenda katika ofisi ya madini ya Kahama kwa ajili ya kupata utaratibu wa umilikaji wa eneo la uchimbaji wa madini na upatikanaji wa leseni.
Akitoa maelezo Katibu wa kikundi hicho alisema kuwa kutokana na juhudi zote na taratibu zilizofanywa na kikunbdi hicho Ofisa Madini Kutoka Kahama,aliyemtaja kwa jina la Nkya, alikubaliana na wanachimbaji hao na kuwataka walipie ada ya upimaji ambayo ilikuwa ni shilingi laki mbili abayo ililipwa kwa viwanja 10 ambavyo ni sawa na heka 50.
Sunday, November 11, 2012
VITA YA MEMBE NA BASHE NI DHAHIRI. BASHE ASEMA MEMBE NI MNAFIKI
MPASUKO ndani ya chama cha Maapinduzi CCM umeendelea kushika kasi jambo ambalo linawafanuya makada wa chama hicho kujikuta wakigawanyika kutokana na makundi hayo ambayo kwa sasa yanashika kasi.
Hali hiyo imejidhiilisha jana baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Husein Bashe kumtuhumu waziwazi,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano waa Kimataifa, Bernardi Membe kuwa ni kati ya wanasiasa wachache ambao wanashiri kutumia makundi ndani ya chama ili kuwachafua wengine.
Bashe akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa alisema kuwa analazimika kumtaja Membe kuwa ni kiongozi mnafiki ndani ya chama kutokana na kutokuwa na msimamao na kujenga chuki kati ya wana CCM wenzake.
Alisema kuwa Membe amekuwa mtaabishaji ndani ya chama kwani amekuwa akifanya siasa za kihuni na za kutengeneza makundi kutokana na hali hiyo Baashe alimtaja Membe kma muhumi, mnafiki na kiongozi ambaye ana sifa ya kushika madaraka ndani ya chama hicho kikongwe.
Bashe alienda mbali zaidi na kudai kuwa Membe amekuwa akiwatumia vibaraka wake ambao kimsingi hawana akiri za kufikiria akiwemo Naaibu Waziri wa Malisili na Utali Lazaro Nyalandu ambaye wanashikiana kufanyua hujuma ndani ya chama cha Maapinduzi.
Hata hivyo alisema kuwa Membe amekuwa na fikra za kukihujumu chama hichjo na kuandaa mazingira ambayo yatasababisha chi kuchukuliwa na upinzani katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Aidha Bashe alisema kuwa inaonyesha wazi kuwa Membe ni mwanasiasa ambaye amezoea kubebwa katika chaguzi mbalimbali na hata amekuwa kiongozi nadani ya CCM akisababbisha kuwepo kwa migongano ikiwa ni pamoja na kufanya siasa za kinafi na uongo ambazo amekuwa akizifanya ndani ya chama na kusababisha migogoro mikubwa hususani katika Jumuiya ya Vijana.
JK ANG'AKA MAKUNDI NDANI YA CCM
BAADA ya Chama Cha Mapinduzi kuonekana kinatajwa kwa kira mara na kujingezea umaarufu wa kutoa rushwa katika chaguzi zake sasa Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye pia ni Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, amefunguka na kutangaza msimamo wa kuwashighulikia wanachama ambao wananunua uongozi kwa kutoa rushwa kwa wajumbe ambao ni wapiga kura.
Kufunguka kwa Mwenyekiti wa chama hicho huyo kunatokana kuwa takribani wiki moja sasa, makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamekuwa wakipigana vita ya wazi dhidi ya kundi linalotajwa kumuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani,Edward Lowassa, linalotaka kufanya mapinduzi ya safu ya juu ya uongozi ndani ya chama hicho.
Makundi hayo yanatokana na mwendelezo wa vita ya makundi hasimu ndani ya chama hicho ambayo yalianza mikakati ya kuhakikisha yanashika nafasi zote nyeti kuanzia ngazi za chini hadi taifa.
Hali hiyo inatokana na kujipanga ama kupanga safi ambayo itaweza kufanikisha uchaguzi mkuu wa ndani wa CCM katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2015.
Duru za uchunguzi za Tanzania Daima wakati mchakato wa kumtafuta Mwenyekiti CCM Taifa zimebaini kuwa, rais Kikwete baada ya kufikishiwa taarifa za kuwepo mpango wa kumpoka nafasi ya uenyekiti kwa kisingizio cha kumpungumzia majukumu unaodaiwa kuratibiwa na kundi la wana CCM wanaomuunga mkono, Lowassa huku lengo halisi la hatua hiyo likiwa ni mkakati wa kundi hilo kujiimarisha katika kutoa mgombea urais kwenye uchaguzi wa 2015, aliamua kuitumia hotuba yake ya jana ya kufungua mkutano mkuu wa nane wa chama kuonya kuhusu jambo hilo na kuwataka wanaoutamani urais kutokiua chama hicho.
Thursday, November 8, 2012
MAKINDA: WABUNGE HAWAJUI KUULIZA MASWALI YA KISERA
KATIKA hali isiyo kuwa
ya kawaida Spika wa bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda amewakemea na kuwabea
wabunge kuwa hawna hoja za kuuliza katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo
kwa Wazri Mkuu kutokana na wabunge wengi kushindwa kuuliza maswali ya kisera.
Makinda alisema katika
kipindi cha Maswali ya Waziri Mkuu wabunge wanatakiwa kuuliza maswali ambayo
yatakuwa ni ya kisera badala ya kuuliza maswali yao ya kijimbo ambayo kimsingi
yanakwenda kinyume na kanuni za kumuuliza Waziri Mkuu maswali.
Kauli ya makinda
imetokana na badhi ya wabunge kushindwa kuuliza maswali ya msingi ambayo alitakiwa
kuulizwa Waziri Mkuu katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo .
Spika alisema kuwa
kimsingi maswali ya leo (Jana) maswali mengi ya wabunge yalikuwa hayaeleweki na
hayakuwa mazuri kwa waziri mkuu na badala yake yalikuwa yakiulizwa kwa
kuzunguka saba bila kwenda moja kwa moja katika swali la msingi.
“Janani wabunge leo
maswali yote yalikuwa mabaya sana wala hayakuwa mazuri kwani wabunge mekuwa
mizungumza kwa kuzunguka na wakati mwingine mlikuwa kushindwa kuuliza, wabunge
mmeshindwa kupanga vizuri maswali yenu lakini sasa mjifunze kuuliza maswali
vizuri ili muweze kuelewa maswali ya msingi” alisema.
Hata hivyo alimtaka
mbunge wa Bukombe Profesa Kulikoyera Kahigi, (Chadema),kumwandikisa waziri Mkuu
Mizengo Pinda kuhusu kuwepo kwa migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na maofisa wa
malisili kuwanyanyasa wananchi ambao wanakadiriwa kufika 70,000.
KAFULILA : CCM INAKIUKA ILANI YAKE
MBUNGE wa Kigoma Kusini David Kafulila
(NCCR-Mageuzi),amemchachafa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa kusema kuwa serikali
inayoongozwa na Chama cha mapinduzi imekuwa ikigawa ikikiuka ilani ya chama
chao ambayo inaelekeza kwa ardhi ni ishara ya ujamaa na badala yake wamekuwa
wakiwabeba mabepari kutoka nchini marekani ambao wanapatiwa ardhi huku wazawa
wakinyanyaswa.
Kafulila aliitoa kauli hiyo jana bungeni bungeni wakati wa
kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, kwa kuhoji ni kwanini
serikali imekuwa ikitumia mfumo wa kibeneru katika ugawaji wa ardhi kwa
wawekezaji na kusahau kuwa ardhi kwa Tanzania ni hishara ya ujaamaa.
Mbali nahilo alitaka kuelewa ni kwanini wawekezaji wamekuwa
wakipewa ardhi kubwa wakati wenyeji wakifukuzwa katika maeneo yao kwa ajili ya
kuwapatia ardhi hiyo wageni hususani pale inapobainika kuwa ardhi hiyo ina
rutuba.
Mbunge huyo alitolea mfano katika jimbo la kigoma kusini ambapo
mwekezaji ambaye alimtaja kwa jina la Agrosol kupewa hekta 10,000 wakati eneo
hilo ambalo alipewa mwekezaji huyo ambapo eneo hilo linakusudiwa kujengwa makao
makuu ya halmashauri.
Aidha alimtaja mwekezaji mwingine kuwa ni FELISA kupewa hekta
3000.jambo ambalo lilipelekea kikosi cha mgambo wa mwekezaji huyo kuwapiga
wananchi na kuwapeleka katika kituo cha jeshi la polisi na kusababisha wakazi
hao kufunguliwa kesi katika mahakama ya mwanzo ya Mwandiga.
Kwa mujibu wa maelezo ya Kafulila alisema kutokana na serikali
kuwa na tabia ya kuwapa kipaumbele wawekezaji wakubwa kupewa ardhi huku wazawa
wanaendelea kutaabika kunaweza kutokea machafuko makubwa ambayo yatakuwa
yamesababishwa na serikali yenyewe.
PINDA: KATIBA MPYA NI KABLA YA UCHAGUZI WA 2015
WAZIRI Mkuu Mizengo
Pinda jana ameliahakikishia bunge kuwa ifikapo uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
tayari katiba mpya itakuwa imekamilika.
Pinda alitoa kauli
hiyo kutokana na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman
Mbowe (Chadema),kuitaka serikali kutoa kauli bungeni ni lini itafanya
marekebisho ya katiba kuhusu kurekebisha daftari la kudumu la mpiga kura.
Mbowe alisema kuwa
kutokana na daftari lakudumu la mpiga kura kupitwa na wakati kunapelekea
watanzania wengi kukosa haki yao ya kupiga kura katika chaguzi mbalimbali
ambazo zinaendelea tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliopita.
Hata hivyo alimtaka
Wazri Mkuu kutoa kauli ya serikali kama kuna mpango wowote wa kufanya
marekebisho ya baadhi ya sheria zinazoongoza uchaguzi iwapo katiba mpya ambayo
inakusudiwa kutumika mwaka 2015 itakuwa bado haijakamilika.
Mbowe alisema kuwa
kuna uwezekano mkubwa wa katiba mpya ambayo inatakiwa kuandikwa na kutumika
katika mwaka 2015 na iwapo marekebisho hayo hayatafanyiwa marekebisho ni ya
sheria ya uchaguzi kuna watu wengi watakosa haki zao za kupiga kura kama
ilinavyojionyesha katika chaguzi ndogo.
Sunday, October 28, 2012
SEHEMU YA PILI YA JACKSON AKIUAGA UKAPELA USIKU HUU UKUMBI WA CHIKAGO BEACH
AHSANTE BABA....
BABA MZAZI WA JACKSON KALUMUNA AKIJISIKIA FAHARI KUBWA BAADA YA KUONA MTOTO WAKE AMEFUNGA NDOA HAPO ANAMPA HONGERA JACKSON KWA MAELEZO ZAIDI NI KUWA BABA YUPO UPANDE WA KUSHOTO NA JACKSON KALUMUNA YUPO UPANDE WA KULIA
UZEE HAUZUII FURAHA ..... BABA YAKE MZAZI NA JACKSON KALUMUNA AKIWA ANACHEZA NGOMA YA KIHAYA KWA FURAHA SANA BAADA YA MTOTO WAKE JACKSON KALUMUNA KUPATA MWENZA WAKE
KAMA UNAJUA KIHAYA OTEA WIMBO GANI UNAIMBWA HAPA: MAMA MZAZI JUDITH KATIKATI AKIWA ANACHEZA NGOMA YA KIHAYA IKIWA NI KATI YA FURAHA BAADA YA AMBAYO IMETOKANA NA JACKSON KUZIKUTANISHA FAMILIA MBILI TOFAUTI
KAKA WA MLIKI WA MTANDAO HUU, AKIWA KATIKA POOOZI NA MY SHEMJIYAKE
HUYU NI BABA MWENYE NYUMBA ANAITWA HON DANSON D KAIJAGE ANAPATIKANA DODOMA TANZANIA.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
WENYE SHUGHULI YAO SASAAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! WANACHEEEKAAAAAAA....
NDANI YA UKUMBI WA CHIKAGO BEACH BWANA JACKSON KALUMUNA AKIWA NA USO WA FURAHA BAADA YA KUPATA UHAKIKAKA KUJIPATATIA JIKO HADI RAHAA... HUYU MDOGO WA MWISHO WA MLIKI WA MTANDAO HUU , BWANA DAN KAIJAGE. |
MDAU JACKSON ANAUGA UKAPELA LEO HII
BWANA HARUSI JACKSON KALUMUNA
BIBI HARUSI MWENYEWE
SIKU YA SEND OFF YA BIBIE
HUYU NI JACKSON KALUMUNA AKIWA AMEPAMBWA NA FEDHAAAA KUTOKA KWA RAFIKI ZAKE WA KANISA LA TAG KAWE WAKATO WA BEG PART JACKSON ANATARAJIA KUPATA MWEZA WAKE JUMAPILI 28/10 MWAKA HUU.
JACKSON KALUMUNA AKIWA ANAONYESHA ISHARA YA UPENDO KWA KUMVALISHA PETE MKE WAKE AGNESS AMBAYE KWA SASA KAACHANA NA JINA LA KIMWELI NA SASA ANATUMIA JINA LA AGNESS J KALUMUNA.
BIBI ARUSI AKIJIBU MAPIGO KWA KUMVALISHA PETE YA NDOA JACKSON KALUMUNA NA SASA AGNESS AMEKUWA MWANA FAMILIA YETU MOJA KWA MOJA KARIBU SAA 12 NA NUSU SASA TUNAELEKEA UKUMBINI KWA KULA UBWABWA NA NDIZI NA KUCHEZA NGOMA YA KIHAYA.
WAZAZI WA BIBI HARUSI KUSHOTO MWENYE TAI ZAMBARAU NI BABA WA BIBI ARUSI NA KULIA NI MAMA WA BIBI HARUSI KUTOKA KIGAMBONI.
HAWA NI NDUGU WA BWANA HARUSI WAKIWA WAMETOKEA DSM, DOM NA BUKOBA KWA LENGO LA KUAKIKISHA NDOGO WAO JACKSON KALUMUNA ANAPATA MWENZA WAKE
WAKIWA NA NYUSO ZA FURAHA BAADA YA KUFUNGA NDOA HAPA KILA MMOJA AKIWA ANAPOKEA PONGEZI KUTOKA KWA WAUMINI WA KANISA LA TAG KAWE JIJINI DSM DUUUUU JACKSON NA AGNESS HONGERA SANA VITA MMEISHINDA
WAZAZI WA JAKSON KALUMUNA WAKIWA MAKINI NDANI YA IBADA ILINAYOSUBIRIWA KUFUNGWA PUNDE NA MCHUNGAJI KIONGOZI WA KANISA LA TAG KAWE KULIA NI MAMA YAKE MZAZI NA JACKSON KALUMUNA NA KUSHITO NI BABA YAKE MZAZI JACKSON KALUMUNA WAMEPENDEZA HAWAJAPENDEZA WACHA WE.
MAMA MZAZI WA MMLIKI WA MTANDAO HUU BI JUDITH, AKIWA NA MKE WA WA MLIKI WA MTANDAO HUU CATHERINE
NANI KAMA MAMA........ HAPA NI BWANA DAN KAIJAGE AKIWA NA MAMA YAKE MZAZI
KAMA ZAMAAAANI WAKATI ULEEEEEEEE..... KILA SIKU MAHABA YANAONGEZEKA....
Friday, October 26, 2012
WANAOTUHUMIWA KUMUUA BARLOW WATAJWA
Majina hayo yametajwa na Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema amesema kuwa simu iliyoporwa ya mwanamama ambaye alikuwa akisindikizwa nyumbani na marehemu ndiyo imesaidia kukamilisha upelelezi huo na wahusika kukamatwa.
Waliotajwa kuhusika na hayo mauaji ni Muganyizi Michael Peter (36) ambaye ametajwa kwamba ndiye aliyemuua Barlow, Chacha Waitare Mwita (50), Magige Mwita Marwa (48), Buganzi Edward Kusuta pamoja na Bhoke Marwa Mwita (42) ambao wote wamekatwa wakiwa Dar es Saalam walipokimbilia baada ya mauaji.
Tuesday, October 23, 2012
Subscribe to:
Posts (Atom)