BAADA ya Chama Cha Mapinduzi kuonekana kinatajwa kwa kira mara na kujingezea umaarufu wa kutoa rushwa katika chaguzi zake sasa Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye pia ni Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, amefunguka na kutangaza msimamo wa kuwashighulikia wanachama ambao wananunua uongozi kwa kutoa rushwa kwa wajumbe ambao ni wapiga kura.
Kufunguka kwa Mwenyekiti wa chama hicho huyo kunatokana kuwa takribani wiki moja sasa, makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamekuwa wakipigana vita ya wazi dhidi ya kundi linalotajwa kumuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani,Edward Lowassa, linalotaka kufanya mapinduzi ya safu ya juu ya uongozi ndani ya chama hicho.
Makundi hayo yanatokana na mwendelezo wa vita ya makundi hasimu ndani ya chama hicho ambayo yalianza mikakati ya kuhakikisha yanashika nafasi zote nyeti kuanzia ngazi za chini hadi taifa.
Hali hiyo inatokana na kujipanga ama kupanga safi ambayo itaweza kufanikisha uchaguzi mkuu wa ndani wa CCM katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2015.
Duru za uchunguzi za Tanzania Daima wakati mchakato wa kumtafuta Mwenyekiti CCM Taifa zimebaini kuwa, rais Kikwete baada ya kufikishiwa taarifa za kuwepo mpango wa kumpoka nafasi ya uenyekiti kwa kisingizio cha kumpungumzia majukumu unaodaiwa kuratibiwa na kundi la wana CCM wanaomuunga mkono, Lowassa huku lengo halisi la hatua hiyo likiwa ni mkakati wa kundi hilo kujiimarisha katika kutoa mgombea urais kwenye uchaguzi wa 2015, aliamua kuitumia hotuba yake ya jana ya kufungua mkutano mkuu wa nane wa chama kuonya kuhusu jambo hilo na kuwataka wanaoutamani urais kutokiua chama hicho.
Rais Kikwete akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano huo ulioanza jana katika ukumbu wa mikutano uliopo Kizota nje kidogo ya Mji huu, Rais Kikwete alianza kwa kuwaonya viongozi wa CCM aliowataja kuwa na ndimi mbili na wale ambao hawatishwi wala kushtushwa na mwenendo mbaya wa chama kuwa hawafai kuwa viongozi.
Rais Kikwete aliamua kupigiria msumari kwa kusema kuwa ndani ya chama cha mapinduzi kuna dalili mbaya za vitendo vya rushwa na kudai kuwa jambo hilo la rushwa halipingiki.
Kikwete akiwa na sura ambayo ni ya tofauti na siku zote kwani mara nyingi upendelea kucheka na kutabasamu mara kadhaa lakini katika hali ya kushangaza muda mwingi wa hotuba yake alionyesha sura ya kukasirika.
Hata hivyo hotuba yake ilionekana kuwalenga moja kwa moja baadhi ya wanaCCM waliokwisha onyesha nia ya kuutamani urais baada ya kipindi chake kumalizika.
Kiongozi huyo wa CCM, alirejea maamuzi yaliyofikiwa na vikao vya juu vya chama hicho ya utekelezaji wa mageuzi ya ndani kwa kueleza kuwa moja ya maazimio ni chama kuchukua hatua dhidi ya viongozi wasio waadilifu na wale wanachafua taswira ya chama.
Rais Kikwete aliwataka wana CCM wenye moyo safi kukabiliana na wale wanaopandikiza chuki ndani ya chama na kuonya kuwa iwapo vitendo vya kuhasimiana havitakoma chama hicho kitadhoofu na uenda kikasambaliatika.
Alibainisha kuwa amegundua chanzo cha kuhamasiana baina ya makada wa chama hicho ni chaguzi za kuwania nafasi za uongozi na ugomvi wa kuwania ukuu wa dola.
“Chanzo cha kutofautiana kwetu ni chaguzi zetu na kutafuta ukuu wa dola. Robo tatu ya migawanyiko na migogoro ndani ya CCM inahusiana na vyeo, sisi ni ugomvi wa urais tu. Wapo ambao wameanza kunihusisha hata mimi na kambi zao, siingii kambi yoyote, niacheni.”alisema.
Alisisitiza kuwa wanaCCM wenye nia ya kuwania uteuzi wa kugombea urais wasifanye hivyo kwa gharama ya kukiua chama hicho na kwamba iwapo vita ya kuwania uongozi ndani ya chama itakwisha, kitakuwa salama.
Wakati rais Kikwete akitoa onyo hilo jana, mikakati ya siri na ya wazi ya kumpigia kura ya hapana katika kuwania uenyekiti imekuwa ikiendeshwa kwa muda sasa kwenye maeneo mbalimbali ya mkoani hapa.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya chama hicho, zimeeleza kuwa mkakati huo umekuwa ukiendeshwa na makada vijana wa chama hicho ambao wamekuwa katika mapambano makali ya kupanga safu za uongozi wa ndani ya chama ili kuliwezesha kundi wanaloliunga mkono kushika ukuu wa dola.
Pamoja na kuwa Rais Kikwete kuwachimbia mkwara wana CCM juu ya vitendo vya Rushwa lakini bado makundi yalionekana kushika kasi katika maeneo ya viwanja vya Kizota mjini hapa.
Hata hivyo, baadhi ya wajumbe bila kujua wanaongea na nani walisikika wakionyesha nguvu kubwa ya kumlaumu Jakaya kwa madai kuwa amekuwa mzungumzaji zaidi badala ya kutenda kile alichokisema.
“Shida ya Mwenyekiti wetu ni msemaji laki si mtekelezaji wa kile anachokisema hata leo ameonekana kuwa mkali lakini si kweli kuwa ataweza kuwachukulia hatua wahusika…..
“Kwani nani asiye wajua wala rushwa ni nani hata yeye anawajua lakini hawezi kuwachukulia hatua yoyote na hali hiyo ndiyo inayosababisha kusababbisha mtafaruku wa chama hiki” alisema.
Huku katia viwanja hivyo mabango yakionekana kushika kasi na baadhi wapiga debe wakionekana kufanya kampeni za kufa mtu na wengine kuonekana kuongelea chemba.
Ili hata hivyo Makada wanaotajwa kuonekana kutengeneza makundi ndani ya CCM ni mtoto Lowassa, Fredy Lowassa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Martine Shigela, aliyekuwa Naibu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa na kada mwingine wa chama hicho, Hussein Bashe.
No comments:
Post a Comment