Pinda alitoa kauli
hiyo kutokana na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman
Mbowe (Chadema),kuitaka serikali kutoa kauli bungeni ni lini itafanya
marekebisho ya katiba kuhusu kurekebisha daftari la kudumu la mpiga kura.
Mbowe alisema kuwa
kutokana na daftari lakudumu la mpiga kura kupitwa na wakati kunapelekea
watanzania wengi kukosa haki yao ya kupiga kura katika chaguzi mbalimbali
ambazo zinaendelea tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliopita.
Hata hivyo alimtaka
Wazri Mkuu kutoa kauli ya serikali kama kuna mpango wowote wa kufanya
marekebisho ya baadhi ya sheria zinazoongoza uchaguzi iwapo katiba mpya ambayo
inakusudiwa kutumika mwaka 2015 itakuwa bado haijakamilika.
Mbowe alisema kuwa
kuna uwezekano mkubwa wa katiba mpya ambayo inatakiwa kuandikwa na kutumika
katika mwaka 2015 na iwapo marekebisho hayo hayatafanyiwa marekebisho ni ya
sheria ya uchaguzi kuna watu wengi watakosa haki zao za kupiga kura kama
ilinavyojionyesha katika chaguzi ndogo.
Aidha kiongozi huyo
alitaka Wazri Mkuu atoe kauli bungeni ni lini marekebisho ya Daftari la kudumu
la mpiga kura litarekebishwa ili kuweka mfumo mzuri ambao unawapa fursa wapiga
kura wote wenye shifa kushiriki.
“Nakumbuka Waziri Mkuu
mnamo 19 Aprili mwaka huu nilikuuliza juu ya kauli ya serikali ni jinsi gani
itarekebisha daftari la kudumu la mpiga kura ili kutoa fursa kwa wapiga kura
wenye sifa kushiriki lakini hadi sasa hakuna sijui kama kuna hatua zozote
ambazo zimechukuliwa” alisema.
Mbowe alisema kama,
katiba itakuwa haijakamilika na kulazimika kufanya uchaguzi kwa kutumia katiba
ya sasa kuna watu ambao watanyimwa haki zao isipokuwa tu kama kutakuwa
kumefanyika marekebisho ya sheria zinazosimamia uchaguzi.
Waziri Mkuu akijibu
swali hilo alisema kuwa hakuna sababu ya mbunge huyo kuwa na wasiwasi kwani ana
uhakika kuwa ifikapo kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2015 katiba mpya itakuwa
tayari na itatumika.
“Mimi sina shaka juu
ya tatiba mpya kuwa tayari mwaka 2015 kwani hata hivi tu nilikuwa na mwenyekiti
wa tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya Jaji Jaji Joseph Warioba na
kunihakikisha kuwa kazi inaenda vizuri…..
“Hivyo mheshimiwa
Mbowe sijui kwanini unakuwa na hofu lakini hata hivyo tunashukuru kwa ushauri
wako kama ikionekana kujitokea kuwepo kwa mapungufu mbalimbali hadi katiba mpya
isiwe tayari basi tutarekebisha sheria zinazosimamia uchaguzi ili kila mmoja
apate haki yake ya kupiga kura” alisema.
No comments:
Post a Comment