MBUNGE wa Kigoma Kusini David Kafulila
(NCCR-Mageuzi),amemchachafa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa kusema kuwa serikali
inayoongozwa na Chama cha mapinduzi imekuwa ikigawa ikikiuka ilani ya chama
chao ambayo inaelekeza kwa ardhi ni ishara ya ujamaa na badala yake wamekuwa
wakiwabeba mabepari kutoka nchini marekani ambao wanapatiwa ardhi huku wazawa
wakinyanyaswa.
Kafulila aliitoa kauli hiyo jana bungeni bungeni wakati wa
kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, kwa kuhoji ni kwanini
serikali imekuwa ikitumia mfumo wa kibeneru katika ugawaji wa ardhi kwa
wawekezaji na kusahau kuwa ardhi kwa Tanzania ni hishara ya ujaamaa.
Mbali nahilo alitaka kuelewa ni kwanini wawekezaji wamekuwa
wakipewa ardhi kubwa wakati wenyeji wakifukuzwa katika maeneo yao kwa ajili ya
kuwapatia ardhi hiyo wageni hususani pale inapobainika kuwa ardhi hiyo ina
rutuba.
Mbunge huyo alitolea mfano katika jimbo la kigoma kusini ambapo
mwekezaji ambaye alimtaja kwa jina la Agrosol kupewa hekta 10,000 wakati eneo
hilo ambalo alipewa mwekezaji huyo ambapo eneo hilo linakusudiwa kujengwa makao
makuu ya halmashauri.
Aidha alimtaja mwekezaji mwingine kuwa ni FELISA kupewa hekta
3000.jambo ambalo lilipelekea kikosi cha mgambo wa mwekezaji huyo kuwapiga
wananchi na kuwapeleka katika kituo cha jeshi la polisi na kusababisha wakazi
hao kufunguliwa kesi katika mahakama ya mwanzo ya Mwandiga.
Kwa mujibu wa maelezo ya Kafulila alisema kutokana na serikali
kuwa na tabia ya kuwapa kipaumbele wawekezaji wakubwa kupewa ardhi huku wazawa
wanaendelea kutaabika kunaweza kutokea machafuko makubwa ambayo yatakuwa
yamesababishwa na serikali yenyewe.
Kutokana na kauli hiyo ilimppelekea Wazri Mkuu Mizengo Pinda
kudai kuwa pamoja na kuwa suala la uwekezaji wa wageni kupewa ardhi kubwa kwake
binafsi siyo dhambi bali kinachotakiwa ni kufuata utaratibu wa utoaji wa ardhi.
Hata hivyo Waziri Mkuu, akijibu swali hilo alisema kuwa
yeye binafsi haoni kama wawekezaji kutoka nje kupatiwa ardhi ni dhambi jambo
ambalo lilizua ubishani kati ya Waziri Mkuu na Kafulila .
Kafulila alisema kuwa yeye mwenyewe anaona wazi kuwa kitendo cha
wageni kupatiwa ardhi kuwa kwa madai kuwa ni wawekezaji wakubwa na wenyeji
kuendelea kunyanyasika ni dhambi kubwa kwani kunaweza kukatokea machafuko
kutokana na wawekezaji hao kuonyesha vitendo vya kuwatharirisha wazawa katika
maeneo yao ambayo wanayapisha kwa ajili ya wawekezaji wakubwa.
Hata hivyo Kafulila alisema ugawaji wa ardhi kwa
wawekezaji wakubwa kutoka nje, uakuwa na mashinikizo makubwa kutoka kwa vigogo
wa serikali kuu hata kama halmashauri zitakuwa zimekaa na kupitisha maamuzi ya
kumkataa mwekezaji huyo.
Hata hivyo Pinda alikiri kuwa suala la ardhi ni suala ambalo
linagusa hisia za watu wengi na hivyo serikali inatakiwa kuzingatia zaidi
vigezo ambavyo vinatakiwa kabla ya kutoa ardhi kwa mwekezaji.
Aidha alielekeza kuwa halmashauri zote nchini zinatakiwa
kushiriki vyema na kuwashirikisha viongozi wote wa serikali za mitaa ili kuweza
kuondokana na matatizo ambayo yanaweza kujitokea na kusababisha kuwepo kwa
mgongano kati ya mwekezaji na wananchi ambao ni wazawa.
Hata hivyo Pinda alisema kuwa kama utaratibu wa kuwapata
wawekezaji utakuwa mbaya ama watanzania watakuwa awapendi kuwepo kwa wawekezaji
wa ardhi ni wazi ardhi hiyo itakuwa mapori ambayo yatakuwa yametapakaa.
“Sawa pamoja na kuwa suala la ardhi linahitaji uangalifu mkubwa
lakini tukiwakataa wawekezaji kutoka nje ni wazi kuwa tutakuta kunayaruka
mapori tu asubuhi hadi jioni” alisema .
Hata hivyo Pinda alimkemea Kafulila na kumtaka aache kumkoromea
na badala yake akaonane na uongozi wa halmashauri kwa ajili ya kupamga
utaratibu wa kutoa ardhi kwa wawekezaji wa ardhi kutoka nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment