KATIKA hali isiyo kuwa
ya kawaida Spika wa bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda amewakemea na kuwabea
wabunge kuwa hawna hoja za kuuliza katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo
kwa Wazri Mkuu kutokana na wabunge wengi kushindwa kuuliza maswali ya kisera.
Makinda alisema katika
kipindi cha Maswali ya Waziri Mkuu wabunge wanatakiwa kuuliza maswali ambayo
yatakuwa ni ya kisera badala ya kuuliza maswali yao ya kijimbo ambayo kimsingi
yanakwenda kinyume na kanuni za kumuuliza Waziri Mkuu maswali.
Kauli ya makinda
imetokana na badhi ya wabunge kushindwa kuuliza maswali ya msingi ambayo alitakiwa
kuulizwa Waziri Mkuu katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo .
Spika alisema kuwa
kimsingi maswali ya leo (Jana) maswali mengi ya wabunge yalikuwa hayaeleweki na
hayakuwa mazuri kwa waziri mkuu na badala yake yalikuwa yakiulizwa kwa
kuzunguka saba bila kwenda moja kwa moja katika swali la msingi.
“Janani wabunge leo
maswali yote yalikuwa mabaya sana wala hayakuwa mazuri kwani wabunge mekuwa
mizungumza kwa kuzunguka na wakati mwingine mlikuwa kushindwa kuuliza, wabunge
mmeshindwa kupanga vizuri maswali yenu lakini sasa mjifunze kuuliza maswali
vizuri ili muweze kuelewa maswali ya msingi” alisema.
Hata hivyo alimtaka
mbunge wa Bukombe Profesa Kulikoyera Kahigi, (Chadema),kumwandikisa waziri Mkuu
Mizengo Pinda kuhusu kuwepo kwa migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na maofisa wa
malisili kuwanyanyasa wananchi ambao wanakadiriwa kufika 70,000.
Profesa Kahigi,alisema
kuwa kwa sasa watu maliasili wamekuwa wakiwakimbiza wananchi katika maeneo yao
kwa ajili ya kupitia mikapa hupya jambo ambalo linasabaisha wanannchi hao
kuishi kama wakimbizi katika maeneo yao.
Kutokana na swali hilo
Spika alimtaka Mbunge huyo kuhakikisha anaandika swali kwa maandishi na
kumpelekea waziri Mkuu ili aweze kushughulikia matatizo hayo kwani Waziri Mkuu
awaezi kulitolea jibu kwa sasa kutokana na kuonekana kuwa ni pipya.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment