Sunday, November 11, 2012

VITA YA MEMBE NA BASHE NI DHAHIRI. BASHE ASEMA MEMBE NI MNAFIKI


MPASUKO ndani ya chama cha Maapinduzi CCM umeendelea kushika kasi jambo ambalo linawafanuya makada wa chama hicho kujikuta wakigawanyika kutokana na makundi hayo ambayo kwa sasa yanashika kasi.
Hali hiyo imejidhiilisha jana baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Husein Bashe kumtuhumu waziwazi,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano waa Kimataifa, Bernardi Membe kuwa ni kati ya wanasiasa wachache ambao wanashiri kutumia makundi ndani ya chama ili kuwachafua wengine.

Bashe akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa alisema kuwa analazimika kumtaja Membe kuwa ni kiongozi mnafiki ndani ya chama kutokana na kutokuwa na msimamao na kujenga chuki kati ya wana CCM wenzake.

Alisema kuwa Membe amekuwa mtaabishaji ndani ya chama kwani amekuwa akifanya siasa za kihuni na za kutengeneza makundi kutokana na hali hiyo Baashe alimtaja Membe kma muhumi, mnafiki na kiongozi ambaye ana sifa ya kushika madaraka ndani ya chama hicho kikongwe.

Bashe alienda mbali zaidi na kudai kuwa Membe amekuwa akiwatumia vibaraka wake ambao kimsingi hawana akiri za kufikiria akiwemo Naaibu Waziri wa Malisili na Utali Lazaro Nyalandu ambaye wanashikiana kufanyua hujuma ndani ya chama cha Maapinduzi.

Hata hivyo alisema kuwa Membe amekuwa na fikra za kukihujumu chama hichjo na kuandaa mazingira ambayo yatasababisha chi kuchukuliwa na upinzani katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Aidha Bashe alisema kuwa inaonyesha wazi kuwa Membe ni mwanasiasa ambaye amezoea kubebwa katika chaguzi mbalimbali na hata amekuwa kiongozi nadani ya CCM akisababbisha kuwepo kwa migongano ikiwa ni pamoja na kufanya siasa za kinafi na uongo ambazo amekuwa akizifanya ndani ya chama na kusababisha migogoro mikubwa hususani katika Jumuiya ya Vijana.

Akizungumzia kile anachosema kuwa Membe ni mnafiki ni pamoja na kuliambia bunge kuwa anawajua mafisadi na wale waliotorosha fedha nje ya nchi laini hadi leo hajaweza kuwa na ujasili wa kutana majina ya watu hao.

Pia alisema kuwa katika uchaguzi mkuu wa jumuiya ya vijana alithubutu kuwatafuta watu ambao ni bibaraka wake kuja katika mkutano wa jumuiya hiyo kufanya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kumtumia Nyalandu kufanya fujo katika mkutano huo.

Aidha alisema kutokana na Membe kutokuwa na sifa ya kuwa kiongozi amedai kuwa kamwe hataweza kumpigia kura yake katika wakati akiomba nafasi ya Unec na kusema kwa atafanya kampeini za kutompigia kura Membe kutokana na kuwa kiongozi ambaye hana mwelekeo.

Alisema kuwa Membe amekuwa akitwatumia vibaraka wake kuwachafua Beno Malisa, Maaartin Shigela, huku akipandikiza chuki kwa vijana ili kuhakikisha chama cha CCM kinadhoofishwa na kuingia mikononi mwa wapinzani.
“Kamwe Membe hawezi kufanikisha mbinu zake chafu na kimsingi nitafanya kampeini ili kuhakikisha hapati nafasi yake ya Unec ambayo anaiwania kwani siasa zake ni chafu zenye kusababisha makundi na machafuko nadani ya chama” alisema .
Akizungumzia tuhuma ambazo zinadaiwa kuwa Bashe, ana mpango wa kufanya kampeini kwa ajili ya kupunguza kura za mwenyekiti wa CCM taifa, akiwa anatuhumiwa kwa kutengeneza vipeperushi Bashe alisema kuwa yeye hausiki na wanaofanya hivyo ni kundi la Membe na waku wake ambao ni wachanga wa kufikiri.

“Membe amekuwa na tabia ya akuzusha mambo ndani ya chama kwani alisha wahi kupeleka maneno ya uongo kwa Rais kuwa mimi nilienda Mtwara kwa ajili ya kuwashawishi vijana kuandaa mabango kwa ajili ya kumzomea Rais pamoja na kumkashifu kambo ambali lilikuwa la uongo” alisema

“Membe amekuwa ni kiongozi ambaye amezoea kuingia madarakani kwa kubebwa sana hata katika kipindi cha kampeini za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 alibebwa na Rostam Azzi kwa kumpatia magari kwa ajili ya kufanya kampeini zake za kijimbo”

Alipouliza kuwa yeye (Bashe ), inasemekana kuwa ni Kibaraka wa Waziri Mkuu Aliyejiuzulu Edward Lowasa, alisema kuwa siyo kweli na Lowasa hajawahi kutangaza kama hatagombea urais katika kipindi hicho cha kugombea uraisi.

Hata hivyo aliweka bayana kuwa iwapo Lowasa atatangaza kugombea atahakikisha anampigia kura kwani hanayo haki kikatiba ya kumchagua mtu ambaye anampenda na mwenye maamuzi ya kuchapa kazi.

“Kama Lowasa atatangaza kuwa anagombea Urais nitampigia kura, kwani Lowasa ni mwana siasa mvumilivu ngani ya chama na ni mzalendo kama angekuwa siyo mvumilivu ni wazi kwa sasa nchi ngekuwa katika sura nyingine, hata mimi nimejifunza mambo mengi kutoka kwake.....
“Kama niliweza kumwombea kura Jakaya Kikwete tena wakati nikiwa nimetoka chuoni hata Lowasa nitamtafutia kura anyingi kwani mamwamini kwa utendaji wake siyo kwa madai kuwa mimi ni kibaraka wake “ alisema Bashe.

Katika hatua nyingine pia Bashe alisema  kuwa tayari ameandika barua  kwa Katibu Mkuu wa Chama hicho inayohusu tuhuma dhidi yake ambazo zilitolewa na Matefy kwenye vyombo vya habari vikimtuhumu moja kwa moja yayey na wenzake.


Alisema kuwa amemwomba Katibu Mkuu wa chama hicho kwa nafasi aliyonayo  na mamlaka  aliyonayo kikatiba  amwite Matefu na kuthibitisha  tuhuma hizo na akishindwa  kuthibitisha tuhuma hizo  hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake.



Vile vile alisema kuwa ikithibitika yeye kuwa yeye Bashe anahusika  na njama hizo  basi hatua kali za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake.



Akizungumzia suala la rushwa ndani ya chama hicho alisema kuwa yeye haamini kama kuna rushwa ndani ya chama kwa kuwa hajawahi kushuhudia hivyo ni vigumu kwa kuthibitisha suala hilo.



Hata hivyo alisema kuwa katika chaguzi zote ni lazima kuwepo na gharama hivyo anaamini kuwa katika chaguzi lazima matumizi ya fedha yawepo.



Kwa upande mwingine tena Bashe alisema kuwa ndani ya chama hicho cha Mapinduzi ambacho ni chama kikubwa hapa nchini  huenda  kukawepo na watu wa aina hiyo wanaojihusisha na rushwa na kukichafua chama.

Vita kubwa inaonekana kuwa katika nafasi 10 za ujumbe wa NEC ambapo mawaziri sita, wabunge watatu, mkuu wa wilaya mmoja, vigogo wawili wa Kamati Kuu ya chama hicho, wafanyabiashara na makada maarufu, ni miongoni mwa wanachama 31 wa Bara watakaonyukana kuzipata.
Hali ni hivyo pia kwa upande wa Zanzibar kwani kati ya wanachama 28 wanaowania nafasi 10 za NEC visiwani humo, wapo mawaziri wanne.
Mawaziri watakaochuana Bara ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Dk. David Mathayo David; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira; Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
Pia wamo Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama na Mbunge wa Iramba Magharibi na Katibu wa Fedha na Uchumi wa CCM, Mwigulu Nchemba. Wote hao ni wajumbe wa Kamati Kuu.
Wengine ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji; Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Martin Shigela na Mbunge wa Nkenge, Assumpter Mshama.
Pia wapo Otieno Peter Baraka, Twalhata Ally Kakurwa, Godwin Kunambi, Innocent Nsena, Richard Tambwe, Anna Magowa, Christopher Mullemwah, Salehe Mhando, Fadhili Nkurlu, Tumsifu Mwasamale, William Malecela, Rashid Kakozi, Luteni Kanali Dk. Kesi Mtambo, Nicholaus Haule na Nussura Nzowa.
Wamo pia Hadija Faraji, Dk. Hussein Hassan, Mwanamanga Mwaduga, Mbunge wa zamani wa Muleba Kaskazini, Ruth Msafiri na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome.
Kwa upande wa Zanzibar, wamo mawaziri wanne akiwamo Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi; Mbunge wa Uzini, Mohamed Seif Khatib; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi; Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Abdallah Juma Sadallah na Waziri wa Fedha, Omar Yussuf Mzee.
Wengine ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha; Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
Wagombea wengine ni Kidawa Hamid Saleh, Abdisalaam Issa Khatib, Khadija Hassan Aboud, Abdalla Ali Hassan, Mohamed Ahmada Salum, Abdulhakim Chasama, Ali Mohamed Ali, Haji Makame Ali, Ibrahim Khamis Fataki, Moza Jaku Hassan, Nassir Ali Juma, Jecha Thabit Kombo, Khamis Mbeto Khamis, Mohamed Hassan Moyo, Bhaguanji Mansuria, Moudline Castico, Yakoub Khalfan Shaha, Rose Mihambo, Ali Omar Mrisho na Mariam Omar Ali.
Wachambuzi wa mambo ya siasa wanasema kuwa, huo utakuwa mkusanyiko mkuu wa aina yake kwani kundi moja litakuwa linalia kwamba limeumizwa na rushwa na lingine litakuwa linafurahia ushindi wa rushwa.
Kitakachowaunganisha ni magwanda yao au fulana zao au kanga zao za kijani na njano, lakini kila mmoja ana hofu, siri na kilio chake moyoni.
Walioshinda kwa rushwa watakuwa wakishangilia ndani ya ukumbi, walioshindwa watakuwa nje wakijaribu kumfikia mwenyekiti wao Kikwete kuomba huruma yake.
Tayari idadi kubwa ya wajumbe wa mkutano huo wameshawasili mjini Dodoma na kusababisha uhaba mkubwa wa nyumba za kulala wageni kwani zote zimechukuliwa na CCM kwa ajili ya mkutano wao huo wa kihistoria.

No comments:

Post a Comment