HALI imezidi kuwa tete katika jeshi la polisi kituo cha Ushirombo kutokana na familia kuapa kulipiza kisasi kwa jeshi la polisi mjini hapo kutokana na mauaji ya kinyama ambayo yaliyofanywa na askari polisi kwa kumfyatulia risasi na kumuua hapo hapo kijana ambaye alifahamika kwa jina la Rashidi Juma (23).
Mauaji hayo ambayo yalifanyika juzi katika maeneo ya Kilima hewa kwa askari wa jeshi la polisi katika kituo cha Ushirombo Mkoani Geita ambaye amefahamika kwa jina la PC Emma G4 tofauti na ilivyokuwa imesemekana kuwa muuaji ni Manase familia kwa sasa imedai kuwa jeshi la polisi linatakiwa kuwajibishwa.
Mauaji hayo ambayo yalitokana na sakata la jeshi la polisi kumshika Mabura Mayala (40)ambaye anatuhumiwa kwa ujambazi kutokana na kujificha kati ya nyumba ambazo zipo maeneo hayo.
Kwa mujibu wa maelezo ya askari polisi pamoja na wananchi zinaeleza kuwa baada ya wananchi kubaini kuwa kuna mtu ambaye walimjengea mashaka walipiga simu polisi kwa lengo la kuomba masaada wa polisi ili akamatwe.
Hata hivyo habari zinasema kuwa baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo wananchi walianza kupiga kelele na kulitaka jeshi la polisi lililohusika na kumkamata mtuhumiwa huyo kumwacha ili wananchi waweze kujichukulia hatua ya kumpiga na kumuua jambo ambalo lisingekuwa rahisi kufanya hivyo.
Kwa mujibu wa shuhuda ambao waliona tukio hilo ndopo askari tajwa alipoamua kumlenga risasi kijana huyo ambaye alimpiga risasi katika sehemu ya nyonga na kumuua hapo hapo.